The House of Favourite Newspapers

Mbowe na Wenzake Wapelekwa Gerezani Baada ya Kushindwa Kulipa Faini

0

Viongozi wanane wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wamepelekwa katika gereza la Segerea kutokana na kushindwa kulipa faini ya Sh 350 milioni.

 

Ni baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani katika mashtaka 12 katika ya 13 yaliyokuwa yanawakabili na kutakiwa kulipa faini hiyo lakini wameshindwa.

 

Uamuzi wa kuwatia hatiani umetolewa leo Jumanne Machi 10, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi.

 

HUKUMU ALIYOTOA LEO HAKIMU THOMAS SIMBA KWA VIONGOZI WA CHADEMA

Kosa la 1 limefutwa
Kosa la 2 wote 10m
Kosa la 3 wote 10m
Kosa la 4 wote 10m
Kosa la 5 Mbowe 10m
Kosa la 6 Mbowe 10m
Kosa la 7 Mdee 10m
Kosa la 8 Heche 10m
Kosa la 9 Mbowe 5m
Kosa la 10 Mbowe 5m
Kosa la 11 Mbowe 10m
Kosa la 12 Mbowe na Msigwa 10m
Kosa la 13 Mbowe na Bulaya 10m
au miezi 5 jela.

 

Leave A Reply