The House of Favourite Newspapers

MBOWE, SERIKALI NGOMA NZITO MAHAKAMNI

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe leo Jumatatu, Novemba 12, 2018 ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa isimfutie dhamana baada ya kusafiri nje ya nchi bila kibali.

 

Mbowe amesema mahakamani hapo kwamba yeye na washtakiwa wenzake ni viongozi na wana majukumu mengi ya kiuongozi ya kutenda ndani na nje ya nchi na kuongeza kwamba anaheshimu sana mahakama lakini mwenendo wote wa Mahakama unawaleta ugumu kufika mahakamani na majukumu yeao nje ya Mahakama.

 

Mbowe amesema mnamo Oktoba 25, 2018 alikuwepo mahakamani wakati lakini vikao vya kamati za bungevilikuwa vikiendelea na leo Novemba 12 wapo Mahakamani wakati Bunge likiendelea.

 

Aidha, kiongozi huyo wa upinzania amesema Oktoba 28, 2018 alisafiri kwenda Washington DC, Marekani kwenye mkutano wa Oktoba 30, 2018 na kwamba kwa ratiba yake alistahili kuondoka huko Oktoba 30, usiku na kurejea Dar es Salaam Oktoba 31 kwa ajili ya kuendelea na kesi Novemba Mosi, 2018.

 

Amedai kabla hajasafiri alipata matatizo ya kuugua hivyo alishindwa kusafiri wala kutibiwa Marekani kwa sababu ya bima ya afya ambayo inaruhusu atibiwe kati nchi za Afrika Mashariki, Afrika Kusini na Dubai.

Hivyo alilazimika kwenda kwenye matibabu katika nchi za Uarabuni na kudai Dubai ndiko aliweza kupata matibabu na amepewa mapumziko lakini atarejea tena huko kwa ajili ya matibabu Novemba 17, 2018.

 

Ameongeza kuwa akiendelea kutibiwa aliona taarifa mbalimbali alizodai ni za upotoshaji kuhusiana na ugonjwa wake na matibabu anapopata kwa ujumla na kuona Mahakama ilivyokwazika kutokana na kutokuwepo kwake.

 

Amesema haikuwa rahisi kwa yeye kutuma taarifa za matibabu kwa sababu bado alikuwa akiendelea na matibabu na taarifa ya ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari na kwamba alipatwa na msiba wa ndugu yake nyumbani kwake Hai Kilimanjaro. Hivyo akaondoka Dubai, Novemba 9, 2018 kwenda Nairobi na hatimaye kwenda Hai Kilimanjaro kuhudhuria mazishi.

 

Mbowe amesema yeye ni mgonjwa wa moyo kwa miaka mingi na ugonjwa huo si homahivyo unastahili uangalizi na pia atawasilisha nyaraka zake za safari, za matibabu, bima ya matibabu kama uthibitisho mahakamani hapo.

 

Wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori amesema amemsikiliza Mbowe akiishawishi Mahakama isimfutie dhamana kwa kukiuka masharti na kwamba hao ni kama washtakiwa wengine wowote na kwamba kwa mujibu wa hati ya mashtaka inayowakabili walipaswa kufuata taratibu za Mahakama na masharti ya dhamana.

 

Watuhumiwa hao walipewa dhamana Aprili, 2018 na kupewa sharti la kufika mahakamani bila ya kukosa na kuripoti Polisi Ijumaa ya kila wiki na kwamba ubunge ni mhimili kama ulivyo Mahakama hivyo ratiba zao zinatakiwa kuendana na ratiba za Mahakama.

 

Naytori amesema ametoa hati ya kusafiria ya Mbowe akionyesha kuwa Novemba 7, 2018 alikuwa Dubai na alitibiwa Novemba 8, 2018. Lakini Novemba 2, 2018 Mbowe alikuwa Brussles Ubelgiji ambapo alitoka Novemba 6, 2018 kwenda Dubai na kudai wanaonyesha hayo kwa sababu ya kuionyesha Mahakama mshtakiwa alikuwa anaumwa anatibiwa Dubai.

 

 

Pia wakili hiyo kuiwasilisha hati ya kiapo kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Salum Hamduni ambaye washtakiwa walipewa jukumu na Mahakama kuripoti kwake kila Ijumaa ya kila wiki.

 

Katika viapo hivyo, wakili huyo amedai mshtakiwa wa kwanza na wenzake hawakwenda kuripoti Polisi kama walivyotakiwa na Mahakama wakati walipewa masharti ya dhamana.

Pia, kuwasilisha kiapo cha Kamanda wa Uhamiaji, Steven Mhina ambaye alimhudumia Mbowe wakati akianza safari na kwamba amedai siku hiyo Mbowe alikuwa mzima na hakusindikizwa na wala hakuwa na msaada wa mtu yeyote.

 

Amedai kamanda Mhina alimhoji Mbowe kuwa anasafiri kwa ajili ya kufanya nini na kwamba akamueleza kwa mapumziko. Viapo hivyo vimewasilishwa mahakamani hapo pamoja na kiapo cha wakili wa Serikali Mkuu, Dkt. Zainabu Mango.

 

Baada ya kueleza hayo, Wakili Nyantori ameiomba Mahakama iwafutie dhamana washtakiwa wote kwa sababu za uvunjifu wa masharti ya dhamana. Sheria ichukue mkondo wake na shauri liendelee kusikilizwa.

 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 23, 2018 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya. Kutolewa uamuzi kama dhamana dhidi ya washtakiwa ifutwe ama la.

MBOWE, SERIKALI NGOMA NZITO MAHAKAMNI

Comments are closed.