The House of Favourite Newspapers

HATIMAYE LULU AMALIZA KIFUNGO CHAKE JELA

HATIMAYE msanii wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amemaliza kutumikia kifungo chake cha miaka miwili jela leo Jumatatu, Novemba 12, 2018 kufuatia kupatikana  NA hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba.

 

Akizungumza na wanahabari baada ya Lulu kumaliza taratibu za kifungo chake, Mkurugenzi wa Idara ya Probesheni Wizara ya Mambo ya Ndani, Aloyce Musika, leo amesema Lulu amemaliza salama na sasa ni raia huru.

 

Novemba 13, 2018 Lulu alihukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia, Steven Kanumba,  lakini tangu Mei 14 mwaka huu, alikuwa akitumikia kifungo hicho cha nje kwa kufanya kazi za usafi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.

 

“Kwa kipindi chote cha kifungo chake, Lulu amekuwa mtiifu, tumekuwa tukimfuatilia nyendo zake, tumeridhika kuwa amebadilika,” amesema Musika.

Comments are closed.