The House of Favourite Newspapers

MBOWE: Waliomuua Akwilina Wapo, Mnataka Kutufunga, Hatuogopi – Video

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (Chadema), Freeman Mbowe, amefafanua kuhusu kinachoendelea juu ya kesi inayomkabili yeye na viongozi wenzake wanane ambayo inasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 23 jijini Dar es Salaam,  amesema wao na pamoja na Chadema kwa ujumla wameonesha kutokuwa na imani na hakimu anayesimamia kesi yao, Wilbard Mashauri,  kwa kile alichosema hakimu hiyo anafanya kazi kwa maelekezo kutoka sehemu fulani yenye lengo la kutowatendea haki na kuwafunga.

 

Mbowe amesisitiza kwamba kinachoendelea kwenye kesi hiyo wanayotuhumiwa kwa makosa 13 likiwemo la kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina, kinajionyesha wazi kwani hata ombi lao la kesi hiyo kusikilizwa Mahakama Kuu limetupiliwa mbali na hakimu ameamuru kesi hiyo inaze kusikilizwa Kisutu leo hiihii,  jambo lililosababisha wakili wao wa upande wa utetezi, Mtobesya,  kujitoa.

 

“Waliomuua Akwilina wapo, lakini tunatengenezewa kesi sisi ili tufungwe, tunasema hatuogopi kwenda jela, lakini tunataka tufungwe pale ambapo tuna haki ya kufungwa. Waue wengine, wapige risasi wengine, waumize wengine, walioonewa ndiyo wanakuwa washutumiwa?” amesema Freeman Mbowe.

VIDEO: MSIKIE MBOWE AKIFUNGUKA

Comments are closed.