Mbunge Abood Atoa Sh. Milioni 2 Kununua Vifaa vya Muziki Kanisa la Mt. Karoli Lwanga
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Dokta Abdulaziz Abood ametoa milioni mbili kwa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Kata ya Mindu, Manispaa ya Morogoro ambapo amesema serikali ipo pamoja na viongozi wa dini na kutambua mchango wao katika suala la kudumisha amani.
Dokta Abood ameyasema hayo wakati alipohudhuria harambee ya kuchangia vifaa vya muziki katika kanisa hilo ambapo Abood ametoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya ununuzi vifaa hivyo vya muziki ikiwa ni jitihada za kuunga mkono viongozi wa dini na kutambua mchango wa waumini wa dini na kanisa hilo.
Dokta Abood amesema serikali inatambua mchango wa viongozi wa dini hivyo wataendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali maendeleo ili kuwasaidia wananchi.
Aidha, Abood amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali wananchi kwenye sekta ya afya ambapo hivi karibuni ametoa magari ya kubeba wagonjwa
“Kuna wakati nikamwambia Mama, Morogoro tuna tatizo la magari kwa ajili ya usafiri wa wagonjwa kwenda Muhimbili, Hospitali Kuu ya Rufaa, na alinipa magari mawili ambayo kwa sasa yamekuwa msaada mkubwa sana.”