The House of Favourite Newspapers

Mbunge Akamatwa Kwa Kumkashifu Rais

0

Mbunge wa Jimbo la Emurua Dikirr nchini Kenya, Johanna Ng’eno amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumkashifu Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake aliyoitoa Jumapili, Septemba 6, 2020.

 

Kwa mujibu wa Gazeti la The Daily Nation, katika hotuba hiyo, Ng’eno akitumia maneno makali yaliyojaa kashfa na matusi, alisikika akimtaka Rais Kenyatta kumaliza mgogoro uliopo baina yake na makamu wake, William Ruto au aondoke madarakani.

 

Hii si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kukamatwa kwa madai ya uchochezi, kwani Septemba 3, 2019 alikamatwa akiwa na mwanasiasa mwingine, Jafferson Langat huku akikamatwa tena Februari 24, mwaka huu kwa madai ya uchochezi.

Leave A Reply