The House of Favourite Newspapers

Mbunge Chadema Atiwa Mbaroni

0

 

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi (CHADEMA) ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Chama mkoani hapo, Rhoda Kunchela anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Mpanda kwa kosa la kukiuka masharti ya dhamana yake.

 

Mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu, Kunchela na Viongozi wengine wa chama hicho walikamatwa na Jeshi la Polisi Mpanda baada ya kuuvamia Mkutano wa hadhara wa Mbunge huyo na wananchi kwa madai ya alifanya mkutano bila kuwa na kibali.

 

Mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Maridadi Kata ya Majengo Manispaaa ya Mpanda, Polisi walivamia na kuchukua computer mpakato (laptop) iliyokuwa ikitumika kurushia matangazo. Mkutano huo ulilenga kusikiliza kero za wananchi kabla ya kwenda Bungeni.

 

Baadaye viongozi hao waliachaiwa na kwa dhamana ambapo miongoni mwa masharti waliopewa ni kuendelea katika Kituo Kikuu cha Polisi Mpanda wakati uchunguzi wa kesi yao ukiwa bado unaendelea.

 

Leave A Reply