The House of Favourite Newspapers

Mbunge Kibaha Vijijini Akabidhi Vitanda na Ambulance 3

0
Magari yaliyokabidhiwa kwa wananchi na mbunge huyo.

 

 

MBUNGE wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa jana alikabidhi magari ya wagonjwa (Ambulance’s) tatu kwa wananchi wa jimbo lake la Kibaha Vijijini.

 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo ya kukabidha magari na vitanda.

 

Magari hayo yamekabidhiwa  kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimio Mlandizi ambapo hafla hiyo ilifanyika na Waziri wa Afya, Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu alikuwa mgeni rasmi na ndiye aliyekabidhi magari hayo.

 

Waziri wa Afya, Jinsia wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza jambo katika hafla hiyo.

 

Akikabidhi zawadi hizo, Ummy alimpongeza mbunge huyo kwa kazi nzuri anayoifanya kwa wananchi wake na akasema anapaswa kuungwa mkono.

 

…Akizindua vitanda hivyo.

 

Alisema juhudi zinazofanywa na mbunge huyo hata serikali ya awamu ya tano inaziona na ndio maana katika magari hayo moja lilitolewa na Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa mbunge huyo katika jamii.

 

Baadhi ya vitanda alivyovitoa mbunge huyo katika hafla hiyo.

 

“Serikali haitasita kuwa bega kwa bega na mbunge huyo katika kumtia moyo hususan anapotekeleza irani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza ahadi zake kwa wananchi,” alisema waziri.

 

Wakitandika mashuka yake.

 

Mbunge huyo alisema ataendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha anawaletea maendeleo na atajitahidi kutimiza ahadi zake kwa kushirikiana na serikali ya CCM. 

Leave A Reply