The House of Favourite Newspapers

DROO YA 5 YA SHINDA NYUMBA… TV, SMARTPHONE, DINNER KUTOLEWA LEO

0
Mwendeshaji wa droo ndogo ya tano ya Shinda Nyumba, MC Chaku akimuelekeza mwanadada kuchanganya rundo la kuponi na kuchagua moja ili kumpata mshindi.

 

WASHINDI wanne waliopatikana katika droo ndogo ya tano ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili iliyofanyika Alhamisi ya wiki iliyopita, watapatiwa zawadi leo katika ofi si za Kampuni ya Global Publishers, zilizoko Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

 

MC Chaku akimpigia simu mshindi wa droo ndogo ya tano ili kumjulisha kuwa ameshinda.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema jana kuwa washindi hao walijinyakulia zawadi za televisheni kubwa, simu moja ya kisasa na seti mbili za vyombo vya nyumbani, watapewa chao kutokana na kuibuka kidedea katika tukio hilo lilifanyika mbele ya mamia ya wasomaji wa Magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi, Amani, Uwazi na Risasi.

 

Kuponi zikichanganywa.

 

“Tunashukuru zoezi zima lilikwenda vizuri na wasomaji walijitokeza kwa wingi katika shughuli hiyo ambayo ilifanyika kwa uwazi wa hali ya juu na uliowavutia wote.

 

Tunawashukuru wasomaji wote kwa ushirikiano mzuri walioutoa na hii inadhihirisha mapenzi yao kwa Global Publishers ambayo siku zote ipo mstari wa mbele kuhakikisha inatoa mchango wake katika kubadili maisha ya watu,”= alisema.

 

Kuponi zikichanganywa.

 

Washindi Waliopatikana katika droo hiyo ndogo ya tano ni Geofrey Shangalawe wa Kigoma aliyejishindia seti moja ya televisheni kubwa ‘flat screen’, Festo Masagasi wa Bunju jijini Dar aliyepata zawadi ya simu ya kisasa ya mkononi, Salome Msaru wa Mtwara na Ummysalama Sasha wa Dar es Salaam ambao kila mmoja alipata zawadi ya seti moja ya vyombo vya nyumbani.

MC Chaku akisoma jina la mshindi.

 

“Tunazidi kuwasisitiza wasomaji wetu kuendelea kusoma magazeti ya Global Publishers ili waweze kubahatika kushinda zawadi mbalimbali zinazotolewa, kabla ya droo kubwa kabisa ambayo mshindi wake atazawadiwa nyumba ya kisasa ikiwa na samani zote.

Mdau akichagua kuponi moja ili kumpata mshindi.

 

“Kama ambavyo nimekuwa nikiwaeleza mara kwa mara kuwa kuponi za kujaza zinapatikana katika kurasa za pili za magazeti ya Ijumaa Wikienda, Risasi, Championi, Amani na Uwazi wakati katika Gazeti la Ijumaa, kuponi zipo katika ukurasa wa tatu, tena mbili kwa mpigo,” alisema Mkanda.

 

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inadhaminiwa na Kampuni ya Premier Bet, Tecno Mobile na Kampuni ya Ving’amuzi ya Ting.

STORI: MWANDISHI WETU

 

Mkazi wa Kigoma Aibuka Kidedea Droo Ndogo ya Tano ya Shinda Nyumba

Leave A Reply