The House of Favourite Newspapers

Mbunge Kuwasaidia Wamachinga Mwanza Kufungua Kesi ya Madai

machi1MANZA: Siku nane baada ya Rais John Pombe Magufuli kuagiza kusitishwa mara moja kwa zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga jijini Mwanza waliokuwa tayari wameondolewa kwenye maeneo yao ya biashara, Mbunge wa jimbo la nyamagana mh.Stanslaus Mabula amefanya mkutano mkubwa wa hadhara na kutangaza kujitolea kuwatafutia msaada wa kisheria kwa ajili ya kufungua kesi ya madai ya mali zao zilizoharibiwa wakati wa operesheni hiyo.

Operesheni hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia Desemba 3 mwaka huu,inadaiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 300 zilizotumika kuandaa maeneo mapya matatu ya Kiloleli,nyegezi na Buswelu walikotakiwa kuhamishiwa wafanyabiashara hao pamoja na posho za askari mgambo zaidi ya 700,askari polisi,askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya jiji la Mwanza na manispaa ya ilemela.

Akihutubia mkutano wa hadhara eneo la igoma sokoni uliokuwa na lengo la kumpongeza Rais Dk.Magufuli kwa jinsi alivyoingilia kati vilio vya wamachinga wa jiji la Mwanza,Mh.Mabula pia amegusia suala la mnada wa ng’ombe wa Nyamatala uliopo wilayani Misungwi,ambao umekuwa ukilalamikiwa kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara ya nyama.

Wakati zoezi la kuwahamisha wamachinga katikati ya jiji la Mwanza likiendelea,wapo baadhi ya watu waliotumia mwanya huo kutekeleza msemo usemao kufa kufaana kwa kuwachangisha wafanyabishara ndogondogo shilingi elfu kumi kila mmoja kwa ajili ya kupewa vizimba kwenye soko la Igoma.

Darassa Afunguka Tuhuma za Kuiba Beat ya Saida Karoli Kwenye Wimbo Wake wa Muziki

Comments are closed.