The House of Favourite Newspapers

Mbunge Mpembenwe Afanya Balaa Tena Kibiti, Ashusha Tena Shehena ya Saruji

0
Mwakilishi wa Kampuni ya PMM Estate 2001 LTD, Deogratius Chacha (mwenye suti bluu bahari) akikabidhi saruji hiyo, Mwenye suti nyeusi ni Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Elius Mpanda.

 

 

MBUNGE wa Jimbo la Kibiti mkoani Pwani, Mheshimiwa Twaha Mpembenwe baada ya kugawa vifaa vya ujenzi katika kata mbalimbali za jimbo hilo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 200 alivyovipata kwa kushirikiana na wadau wake nje ya mfuko wa jimbo, jana Jumanne alipokea tena mifuko 300 ya saruji kutoka kwa rafiki zake wa Kampuni PMM Estate 2001 LTD kwa ajili ya kuendelea kuijenga Kibiti Mpya.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibiti, Mohammed Mavura akitoa shukrani zake baada ya kupokea saruji hiyo.

 

 

Akizungumza wakati wa kupokea saruji hiyo, Katibu Mwenezi Wilaya ya Kibiti, Suleiman Ndumbogani alisema mbunge huyo alikuwa kwenye majukumu ya kikazi jijini Dodoma na kuongeza kuwa msaada huo umefuatia mkutano wa mbunge huyo aliouitisha tarehe 26 mwezi uliopita na kuwakaribisha wadau wake wa kimaendeleo ambao walimuahidi misaada mbalimbali kwa ajili ya jimbo hilo.

Mwenyekiti wa UWT Pwani, Farida Mgomi akishukuru kampuni ya PMM Estate 2001 LTD na Mbunge Twaha Mpembenwe kwa ushirikiano wao wa kimaendeleo baada ya kupokea msaada huo.

 

 

Miongoni mwa waliomuahidi misaada hiyo ni kampuni inayojishughulisha na shughuli za bandari kavu ya PMM Estate 2001 LTD inayoongozwa na Mwanamama, Judith Mhina ambaye aliahidi kusaidia mifuko 600 ya saruji na vitanda kwa ajili ya hosteli za wanafunzi wakike kwenye jimbo hilo ambapo katika hafla hiyo alikuwa akitimiza sehemu ya ahadi yake.

Viongozi wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kibiti, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohammed Mavura (katikati mwenye miwani) wakiwa kwenye picha ya pamoja.

 

 

 

Misaada hiyo ilikabidhiwa na mwakilishi wa kampuni hiyo, Deogratius Chacha aliyemuwakilisha mwanamama Judith Mhina na kupokelewa na Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo ikiongozwa na Abdul Jabir na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibiti, Mohammed Mavura na wengineo.

Lori lenye saruji hiyo likiwa na shehena hiyo stendi ya Kibiti.

 

 

Viongozi wengine walioshiriki kupokea msaada huo ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Elius Mpanda, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Pwani Farida Mgomi, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya hiyo Hamis Kiloko na wengineo.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kibiti, Suleiman Ndumbogani akitoa muongozo kwenye tukio hilo.

 

 

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibiti Mohammed Mavura aliishukuru Kampuni ya PMM Estate 2001 LTD kwa msaada huo na pia alimshukuru mbunge Mpembenwe kwa ukaribu wake na wafadhili wanaomsaidia kulijenga jimbo la Kibiti.

Mwakilishi wa Kampuni ya PMM Estate 2001 LTD, Deogratius Chacha aliyemuwakilisha mmiliki wa kampuni hiyo, Judith Mhina akieleza lengo la kumsapoti mbunge Mpembenwe katika harakati za kimaendeleo.

 

 

“Niishukuru kampuni hii lakini pia nimshukuru mbunge Mpembenwe kwa jitihada zake na urafiki na watu anaoshirikiana nao kuijenga Kibiti.

 

 

“Niwape hongera wananchi mliomchagua mbunge huyu mwenye marafiki wenye moyo wa kumsaidia katika kuleta maendeleo ya Kibiti.

 

 

“Si kila mbunge anaweza kupata marafiki kama hawa wa kumsaidia kulijenga jimbo lake lakini mbunge Twaha Mpembenwe yeye ndani ya kipindi cha miezi tisa tangu achaguliwe ameshatoa misaada yenye thamani ya zaidi ya milioni 200 kutoka kwake na wadau wake na si kwenye mfuko wa jimbo kama wanavyotegemea wabunge wengine.

 

 

“Hivyo niwapongeze tena Wanakibiti kwa kumchagua mbunge kama huyu kwa maendeleo yao”. Misaada hii itakwenda kuboresha katika sekta za kijamii kama vile ujenzi wa zahanati, shule na sehemu nyingine”, alimaliza kusema mkurugenzi.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL 

Leave A Reply