The House of Favourite Newspapers

Mbunge Shigongo ,Tabasamu Waisambaratisha ,Chadema, CUF Buchosa.

0

Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza Eric Shigongo wa Jimbo la Buchosa na Hamis Tabasamu wa Jimbo la Sengerema wamevisambaratisha vyama vya upindanzi vya Chadema ,na CUF wilayani humo baada ya viongozi na Wanachama wa Vyama hivyo kuvihama na kujiunga na CCM.

Kaimu katibu wa CCM wilaya ya Sengerema Adamu Itambu amesema huu ni mwanzo wa kuvuna Wanachama kutoka vyama pinzani kutokana na CCM kuwa chama imara kinachopendwa zaidi hapa nchini.

Wanachama wapatao 30 wa Vyama vya CUF na Chadema wamehamia CCM kwenye mkutano mkuu wa Jimbo la Buchosa ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo Hilo Eric Shigongo kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM miongoni wa waliohamia CCM ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Buchosa Boniphace Kadinda.

Kadinda amesema kuhamia CCM kumetokana na kukoshwa na utendaji kazi wa Serikali wa kuwaletea wananchi maendeleo kwa vitendo hivyo hoja za wapinzani zimejibiwa kwa vitendo na hakuna jipya litakalowafanywa na wapinzani kuwaeleza wananchi waamini sera za vyama pinzani.

Kwa upande wake Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amewaomba wananchi wa Jimbo la Buchosa kuachana na propaganda zinazotolewa na Wapinzani kuhusu uwekezaji Bandari kuwa nchi imezwa na kusema jambo hilo kuwa uzushi.

Hivyo amewaomba wananchi kwa ujumla kuachana na propaganda hizo na kuiamini CCM na Serikali yake kuwa inania ya dhati katika suala Zima la uwekazaji wa Bandari unafaida katika Taifa letu.

” Tunapoona wana CUF Chadema wanahamia CCM mjue wanahama kutokana na kuchoshwa na propaganda za kugawa Taifa tusimame imara na kuitetea nchi yetu, amesema Shigongo.

Huku mbunge wa Sengerema Hamis Tabasamu aliyekuwa mwalikwa kwenye mkutano huo aliwaambia wananchi kuwa wawe na Imani na viongozi wao kuwa maendeleo watapata kupitia Serikali yao.

Sambamba na hilo amewataka CCM kujibu hoja za wapinzani kwa hoja kutokana na CCM kuwa imara kutekeleza Ilani kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Kikao cha Halmashauri ya CCM Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kimepitisha azimio la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kuwa kutekeleza wa Ilani ya CCM kwa vitendo.

Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya Sengerema wamesema hawako tayari Taifa kugawanywa na watu wachache ambao hawalitakii mema Taita.

Leave A Reply