The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Kibiti Atoa Makazi Yake Kusaidia Waathirika wa Mafuriko

0
Mbunge wa Jimbo la Kibiti, mkoani Pwani, Mhe. Twaha Mpembenwe ametembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya wakazi wa jimbo hilo walioathirika kwa mafuriko.
Katika ziara hiyo iliyofanyika jana, Mhe. Mpembenwe alisema kuwa tayari serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia WANANCHI hao ikiwa ni pamoja na msaada wake binafsi kama mbunge, kama sehemu ya faraja kwao
“Serikali imeshatoa fedha kwaajili ya kuwasaidia waathirika, misaada hiyo ipo kwa mkuu wa wilaya,  taratibu muhimu zinafanyika ili kuwasaidia kwa haraka.
“Mimi kama mbunge nimetoa msaada wa vitu mbalimbali muhimu katika mahitaji yetu ya kila siku, ikiwemo chakula na vitu vingine muhimu,” alisema Mhe. Mpembenwe na kuongeza;
“Bado wito wangu kwenu ndugu zangu, nawaombeni tutoke huku tukajihifadhi katika maeneo ambayo serikali ya wilaya imeelekeza, lakini hata nyumbani kwangu pale karibuni sana, tuje tubanane huku tukiangalia taratibu zingine, ” alisema Mhe. Mpembenwe.
Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kupelekea kujaa kwa mto Rufiji na maeneo mengine ya karibu, katika wilaya za Kibiti na Rufiji.
Leave A Reply