The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Uingereza Auawa kwa Kuchomwa Kisu

0

Mbunge wa Southend Magharibi kutoka Chama cha Conservative nchini Uingereza, Sir David Amess amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu katika eneo la Kanisa huko Leigh-on-Sea, Essex.

 

Polisi nchini humo imesema kijana mwenye umri wa miaka 25 amekamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo baada ya shambulio hilo.

Walisema walikuta kisu na hawamtafuti mtu mwingine yeyote kuhusiana na tukio hilo. Sir David, 69, alikuwa mbunge tangu 1983 na alikuwa na mke na watoto watano.

 

Katibu wa Afya Sajid Javid amesema alikuwa; “Mtu mzuri, rafiki mkubwa, na mbunge mzuri, aliyeuawa wakati anatimiza jukumu lake la kidemokrasia”.

 

Leave A Reply