The House of Favourite Newspapers

Mbwa Mwenye Masikio Makubwa Zaidi Duniani Avunja Rekodi

0

TUMEZOEA kuona binadamu wakiweka rekodi mbalimbali, lakini mara hii tunashuhudia mbwa anayejulikana kwa jina Lou akiweka Rekodi ya Dunia ya Guinness baada ya kutangazwa kama mbwa mwenye masikio marefu zaidi duniani, upo hapo?

 

Wanamtandao walishangazwa na mbwa huyo anayemilikiwa na Bwana Paige Olsen kutoka Milwaukee nchini Marekani huku wengine wakimtania kuwa  mnyama huyo ana uwezo wa kusikia kila kitu kutoka mbali. Lou ana masikio yenye urefu wa inchi 13.38 kwa kila sikio.

 

Walichokiandika Guinness kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu mbwa huyo:

“Ana masikio yote! Mbwa huyu anashikilia rekodi mpya kama mbwa mwenye masikio marefu, huyu ni Lou, mbwa mwenye rangi nyeusi na hudhurungi aina ya Coonhound kutoka Milwaukie, Oregon, nchini Marekani. Masikio ya Lou yana urefu wa sentimita 34 (inchi 13.38 ) yote, kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha #GWR2022 wiki hii.”

Mmiliki wa mbwa huyo pia alifurahia rekodi hiyo ya swahiba wake akisema:

“Lou anaweza kufikiria ni mbwa maalum lakini nadhani alifikiria hivyo kutokea mwanzo. Nafikiri amekuwa akijihisi kuwa bora kuliko sisi sote. Sasa watu watakuwa na hamu ya kupiga naye picha. Ninamfurahia sana rafiki yangu mdogo kwa kuwa mbwa maalum.”

 

Maoni ya mtandaoni;

@Sudiksha Kumar alisema: “Natafakari anavyojaribu kula chakula bila kusikia, mbwa huyu anaweza kusikia watu wakifungua suti wakiwa mbali.”

 

@Carmelo Alim Acibar alisema: “Kidogo tu na mbwa huyu atapeperuka.”

@Michelle Barone: Hauwezi kuficha siri.”

 

Leave A Reply