The House of Favourite Newspapers

Mbwa wa Wema kufuru!

0

4mbwa (1)

Mmoja wa Mbwa anaofugwa na Wema.

Musa mateja
KUFURU! Mbwa wanaofugwa na bosi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu, wamedaiwa kufikisha gharama ya Sh. milioni 20 tangu alipoanza kuwafuga ikiwa ni karibia miaka miwili.

Chanzo cha habari hii kilieleza kuwa mbwa hao wamekuwa wakitumia shilingi laki mbili kwa wiki gharama ambayo ni kubwa ambapo itafikia kipindi Wema kama uzalishaji wake utakuwa mdogo basi huduma za mbwa hao anaweza kuzisitisha siku yoyote na kulazimika kuwagawa au kuwauza.

wema_sepetu991Bosi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu.

Wema alianza kuwamiliki mbwa hao mwaka 2014, ambapo alianza na mmoja, ila kutokana na kuzaliana sasa wamefika nane, gharama ya kuwahudumia inaweza kuzidi baada ya mbwa hao kufikia umri wa kuanza kula.

“Dah, nikwambie ndugu yangu saa nyingine Wema anajizidishia gharama za maisha kwa kujitakia maana nimekuwa nikifuatilia kwa wiki moja amekuwa akiwanunulia mbwa wake chakula cha laki mbili ambacho wanatumia kwa muda wa wiki moja tu, pesa hiyo kwa mwezi ni sawa na laki nane na kwa mwaka ni pesa ndefu sana! Inacheza kwenye milioni 20 sasa,” kilisema chanzo hicho.

Wema hakupatikana hewani kufafanua ishu hiyo.

Leave A Reply