The House of Favourite Newspapers

Samatta Atembelea Global Group, Aomba Mashabiki Wafurike Taifa (Picha +Video)

Hali ilivyokuwa wakati Samatta anawasili Ofisi za Global Group Sinza-Mori jijini Dar es Salaam leo.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania,  Mbwana Samatta, leo amezitembelea  ofisi za Global Group  ambapo pamoja na kufanya mahojiano kuhusu mafanikio yake katika soka, ametaka mashabiki wa mchezo huo kufurika Uwanja wa Taifa kesho kwa ajili ya mechi itakayokutanisha timu teule  yake na ya mwanamuziki maarufu nchini, Alikiba.

Wafanyakazi wa Global Group wakijiandaa kumpokea Samatta.

Akifanya mahojiano na +255 Global RadioSamatta alitolea ufafanuzi kwa namna ambavyo alipata wazo la kuanzisha Samakiba Foundation ambayo kesho itakuwa inachezwa kwa msimu wa pili katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo alisema lengo kubwa  ni kurudisha kitu kidogo kwa jamii kupitia soka na alimuona Alikiba kama mtu sahihi wa kushirikiana naye.

…Akisalimiana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Richard Manyota (kushoto) wakati alipowasili ofisi za Global Group. Wa pili kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers na kulia ni Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Ally Salehe ‘Jembe’.

“Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya watu ambao wana mahitaji kwani pesa zitakazopatikana zitakwenda moja kwa moja kwao, hivyo naomba mashabiki waje kwa wingi ili waweze kutusapoti katika kufanikisha jambo hili,”alisema Samatta.

Mfanyakazi wa Global TV,  Jane Moses, akimkabidhi shada la maua Samatta.

Amewataja baadhi ya wachezaji ambao wataunda kikosi chake kuwa  ni pamoja na Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Kelvin John ‘Mbappe’,  Hassan Kessy, Mrisho Ngasa, Athuman Idd ‘Chuji’ na nyota wengine kibao. kutoka Ligi Kuu.  Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni na kiingilio ni Sh.  2,000 kwa mzunguko.

…Akiwa na shada la maua wakati wa chereko za kumpokea.
…Akisindikiwa na wafanyakazi.
Mshambuliaji nyota wa mabingwa wa ligi ya Ubelgiji, klabu ya Genk na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta akiwa tayari kufanya mahojiano na +255 Global Radio leo katika studio zilizopo katika jengo la Global Group Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Samiya Suleiman, mtangazaji wa kipindi cha watoto kiitwacho ‘Kids and Play’ cha +255 Global Radio.
Saleh Ally akiwa tayari kwa mahojiano na Mbwana Samatta.
…Akiwa katika ofisi za Global TV na Abdallah Mrisho na Saleh ‘Jembe’.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

Comments are closed.