The House of Favourite Newspapers

MC Nassa Chipukizi Tishio Kwa Mastaa Wa Singeli

0
Mc Nassa kwenye pozi.

Pande za Mdaula mkoani Pwani na vitongoji vyake mkali wa michano ya singeli, Nassibu Stephene a.k.a Mc Nassa ndiyo habari ya pande hizo.

Vigodoro vyote pande hizo bila Mc Nassa hawajapiga kelele kwa Nassa akee.

Mkali huyo hivi karibuni ametoa ngoma nne zilizomfanya azidi kubamba ambazo ni Mazoea, Subira, Haiwezekani na Dolidoli.

Mkurugenzi wa BEZ-LI Production, inayomsimamia Mc Nassa, Samwel Chilijila a.k.a Mr Target

Akizungumza na mwanahabari wetu Mc Nassa amesema licha ya kutamba pande za Mdaula lengo lake ni kuwafunika mastaa wote wa singeli hapa nchini akiwemo, Shoromwamba, Man Fongo, Mzee wa Bwax na wengineo.

Man Fongo

Pamoja na yote mkali huyo wa singeli amesema lengo la ngoma zake ni kufikisha ujumbe mzuri kwa jamii pamoja na radha tamu ya muziki huo. Akizungumzia mafanikio yake, Mc Nassa amesema yametokana na menejimenti bora ya BEZ-LI Production chini ya Mkurugenzi wake, Samwel Chilijila a.k.a Mr Target na Meneja wake Manka Mushi.

Mzee wa Bwax
Leave A Reply