The House of Favourite Newspapers

Mch. Msigwa Atolewa Gerezani, Azua Balaa – Video

0

RAIS  John Magufuli jana (Alhamisi) Machi 12, 2020, alimlipia Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kiasi cha Tsh milioni 38 kati ya Tsh milioni 40 alizotakiwa kulipa kama faini ili atoke jela kutokana na hukumu iliyopitishwa mapema wiki hii na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 

Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa, amesema kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya ndugu kuchanga na kupata milioni mbili tu na hivyo kumtafuta Magufuli ili kupata msaada huku chama chake cha Chadema nacho kikimlipia faini hiyohiyo ya Tsh milioni 40.

 

Hata hivyo, baada ya kuachiwa huru jana hiyo  katika Gereza Segerea, Mchungaji Msigwa alikataa kupanda gari la serikali baada ya kulipiwa faini.


Awali kulitokea mzozo kati ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Humphrey Polepole ambao walitaka Msigwa apande gari ya serikali kwa kuwa amelipiwa faini yake na Rais Magufuli, lakini wafuasi wa Chadema wakataka apande gari aliloandaliwa na Chadema kwa kuwa chama hicho ndicho kimemlipia faini kupitia michango ya Watanzania.

 

Wafuasi hao walidai kwamba wakati  Magufuli anapeleka fedha tayari Chadema ilikuwa imeshamlipia Msigwa na hivyo fedha hiyo irudishwe kwa rais ili ikafanye shughuli nyingine za maendeleo.

 

Msigwa alilikacha gari  la serikali, akachomoka hadi nje ya gereza walikokuwa wafuasi wa Chadema kisha kupanda na kuelekea makao makuu Kinondoni.

 

Leave A Reply