The House of Favourite Newspapers

Mchezaji Yanga Amkataa Balinya

Ally abdulkarim maarufu kwa jina la Ally sonso(kushoto) akiwa na Juma Balinya (kulia)

ALIYEWAHI kuwa mchezaji wa Yanga, Ally Mayay Tembele, amelitaka benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera, kuhakikisha inafanyia kazi mapungufu yaliyo katika safu ushambuliaji.

 

Yanga wanavaana na Zesco Septemba 15, mwaka huu katika mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga wamefika hapo baada ya kuitupa nje Township Rollers kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mayay ameeleza Yanga haikufanya vizuri walipocheza na Rollers, akisema kwa namna wanavyocheza mbele wanaweza wakashindwa kupata matokeo mazuri kama kocha hatarekebisha safu ya ushambuliaji.

 

“Yanga bado ina mapungufu mengi katika idara ya ushambuliaji, na hilo limekuwa tatizo kwa timu nyingi hapa Tanzania.

 

“Ni vyema kocha akajaribu kulitazama tatizo hili kwa jicho la tatu ili kuongeza makali na umakini timu iweze kufanya vizuri, uwepo wa wachezaji kama Juma Balinya, Patrick Sibomana unahitaji muda kujenga muunganiko wa safu nzuri maana bado ni wageni, kwa sasa unaweza kusema bado hawajawa safi,” alisema Mayay ambaye majeruhi yalimlazimisha kuachana na soka na kurudi chuoni enzi zake.

 

Aidha, kwa upande mwingine Mayay ameeleza katika nafasi ya ulinzi Yanga haina matatizo kama ilivyo mbele hivyo uwepo wa Kelvin Yondani utaisaidia kuzuia makali ya Zesco kutokana na uzoefu wake.

George Mganga, TUDARCo

Comments are closed.