The House of Favourite Newspapers

Mchicha wa Nazi kwa Kula na Ugali

LEO tutaona jinsi ya kupika mchicha wa nazi ambao ni mtamu kwa kula na ugali.

MAHITAJI:

lMchicha mafungu mawili.

lKitunguu na nyanya.

lTui la nazi moja.

 

JINSI YA KUPIKA:

Chukua mchicha, umenye kutoa nyuzinyuzi, baada ya hapo uoshe vizuri kuhakikisha mchanga wote umetoka.

Ukimaliza ukatekate vizuri, katakata kitunguu na nyanya zako.

Baada ya hapo, weka mafuta kiasi kwenye sufuria, kaanga kitunguu na nyanya, vikiiva, weka mchicha, uache uive kidogo kisha weka tui la nazi zito, uache uchemke ili tui lako liive vizuri.

Baada ya hapo mchicha wako utakuwa tayari kwa kuliwa na uga.

Comments are closed.