Mchungaji Afariki Dunia kwa Kufunga Kula Siku 30

MCHUNGAJI Brighton Samajomba wa Kanisa la Heaven Is My Home la nchini Zambia, amefarki dunia siku ya 20 baada ya kupatwa na utapiamlo akiwa kwenye mfungo wa kutokula wa siku 30.

Akihojiwa na mtandao wa Zambia Watchdog, kaka wa marehemu aitwaye Reagan Samajomba, amesema ndugu yake alikuwa na kawaida ya kufunga na kufanya maombi mara kwa mara.

Kuhusu kifo chake, ameeleza kuwa aliamua kufunga siku 30 kwa lengo la kuiombea familia yake na waumini wa kanisa lake.

“Alifariki jana (Jumatano, Septemba 4) akiwa amefikisha siku 20.  Kifo chake ni funzo kwetu, kama familia tunaamini amekufa kwa ajili yetu na kwa imani yake atafika peponi,” amesema.

Polisi mjini Solwezi wamethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaonya wananchi wawe makini na imani zao.


Loading...

Toa comment