The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Mgogo Apata Ajali, Aonywa

0

BAADHI ya Watanzania wamemuomba Mchungaji wa Kanisa la Baptist Tanzania, Daniel Andendekyse Mgogo kutoendelea na hulka ya kuendesha gari mwenyewe hususani katika safari za mbali ili kuepuka ajali inayoweza kuhatarisha maisha yake binafsi.

 

Ombi hilo limekuja siku moja baada ya Mchungaji huyo maarufu katika uinjilishaji, kupata ajali jana mchana maeneo ya Korogwe mkoani Tanga wakati akielekea Dar es Saam akitokea Arusha.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kupitia ukurasa wake wa instagram ilisema “Mchungaji huyo alikuwa peke yake lakini Mungu ni mwema kwani hakuumia wala kujapata majeraha yeyote tunamshukuru Mungu licha ya gari aliyokuwa akiendesha kuharibika vibaya… ashukuriwe Mungu atendaye makuu.”

 

Baada ya taarifa hiyo, baadhi ya wadau akiwamo mcluvanda_events alisema  “Uchovu utakuwa umechangia. Next time don’t drive alone baba. Mungu ni mwema thoug”.

 

Pia mercy_vibubusolutions aliunga mkono hoja hiyo na kusema watumishi wanatakiwa waendeshwe kwa sababu safari za mbali wanakuwa wamechoka… unakuta kahubiri week nzima, kufunga, kuomba lazima mwili uwe dhaifu!

 

Naye hawacostantine alisema Fatigue yaani uchovu ndio umechangia.  Vilevile dr.samsasali360  aliandika ”ashukuriwe Mungu….kuna kausingizi fulani hivi katakuwa kamechangia…yaani kama uko macho kama umelala”.

Cc; mushigabriel

Leave A Reply