The House of Favourite Newspapers

Shigongo: Wanasema Magufuli Aliwadhibiti, Nitashikilia Shilingi – Video

0

MBUNGE wa Buchosa (CCM) ameipongeza Serikali kwa kuhakikisha umeme unapatikana kwa asilimia kubwa, ambapo ameitaka kuendelea kuwekeza kwenye nishati ya umeme.

 

“Shigongo amesema wananchi wa visiwa vya Maisome na Kome wanatumia umeme wa watu binafsi ambao wanawauzia wananchi maskini kwa Tsh 2,400 kwa uniti moja ilihali Serikali ilielekeza wauze Tsh 100 kwa uniti 1.

 

“Wamepandisha bei wanasema Hayati Magufuli alikuwa amewadhibiti, hawajui kama Rais Samia ni moto mkali. Mheshimiwa Waziri kama hutakuja na majibu ya kupunguza bei hiyo kama serikali ilivyoelekeza nitashikilia shilingi.

 

“Tukiwa na nishati hakuna atakaetutisha, uchumi wetu utakua, tunao uwezo wa kuwa Africa Power House, tusiwasikilize wazungu….” Mbunge wa Buchosa, Mhe Eric Shigongo.

 

Aidha, Shigongo amesema baadhi ya maeneo katika jimbo lake hayana umeme na hata yale yenye umeme upo maeneo ya senta tu lakini vijijini ndani hakuna umeme kuna nguzio pekee, hivyo wizara inalo jukumu la kuhakikisha wananchi hao wanapata umeme.

Leave A Reply