The House of Favourite Newspapers

Mdogo wa Mkurugenzi Global azikwa Bupandwamhela

0

1-001Baadhi ya watoto wa marehemu wakiongozwa na baba yao mkubwa, Eric Shigongo, wakipita kuuaga mwili wa mpendwa wao.
2-001Baadhi ya dada wa marehemu wakipita mbele kutoa heshima za mwisho kwa ndugu yao.

3Baadhi ya wakazi wa Bupandwamhela wakiwa na huzuni msibani.

4Jeneza lenye mwili wa Daud likipelekwa makaburini.

5.

6Mama mzazi wa marehemu Daud aitwaye, Ngw’anamaduka (wa kwanza mbele) akiwa katika majonzi.

7.

8Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste, John Swakala (kulia) akitoa ibada fupi kabla ya maziko.

9Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (wa tatu kulia) akiwa katika picha pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wastaafu wa wilaya ya mpya ya Buchosha baada ya kumalizika maziko.

10Jeneza likiandaliwa tayari kwa maziko.

11Mwenyekiti Mstaafu Jumuiya ya Serikali za Mitaa zinazohusika na Ziwa Victoria Afrika Mashariki wa Wilaya ya Sengerema, Metthew Lubengeja (kushoto) akiweka  udongo kaburini.

12Eric Shigongo akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu.

13Mkurugenzi wa Global Publishers, Lydia James,  akiweka udongo kaburini.

14Mkurugenzi wa Global, Marsha Bukumbi, akiweka udongo kaburi la mdogo wao.
15
16     Mmoja wa wanandugu wa familia ya Mzee Zabron aitwaye Yakub Abdallah akishiriki kuweka udongo kaburini.

17Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula, ambaye ni mjomba wa marehemu akishiriki kuweka udongo kaburini.

18Wazazi wa marehemu mzee Zabron na mkewe wakiweka mashada ya maua.

19Baadhi ya kaka wa maerehemu wakiweka mashada ya maua.

20Dada wa marehemu wakiweka mashada.

21 Diwani wa Kata ya Bupandwamhela, Masumbuko Bupamba, akizungumza jambo.

   MDOGO wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo aitwaye Daud Zabron, ambaye alikuwa mtoto wa baba yake mdogo, alizikwa Machi 30 mwaka huu na ndugu,  jamaa na marafiki  kijijini kwao Bupandwamhela-Sengerema, Mwanza.

Marehemu Daud alifariki Machi 29 mwaka huu alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema na kuzikwa nyumbani kwao Bupandwamhela.

Kabla ya maziko hayo kulitanguliwa na ibada fupi iliyoongozwa na Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste, John Swakala,  aliyetoa ibada fupi na baadaye kaka wa marehemu, Eric Shigongo,  aliyetoa neno la shukrani kwa niaba ya familia kwa waombolezaji waliokuwa wamehudhuria msiba huo.

Na Denis Mtima aliyekuwa Buchosa.  

Leave A Reply