The House of Favourite Newspapers

Mdogo wa Rostam Aziz Kortini Kwa Meno ya Tembo, Silaha, Utakatishaji Fedha

Mfanyabiashara, Akram Azizi Abdul Rasool  ambaye ni mdogo wa Rostam Azizi ambaye ni mdogo wa Rostam Azizi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na makosa 75, ikiwemo kukutwa na Nyara za Serikali na utakatishaji fedha kiasi cha Dola za Marekani 9018.

Akram anakabiliwa na kesi ya uhujumu namba 82/2018 ambapo katika makosa yake mawili, anatuhumiwa kukutwa na nyara za serikali, makosa 70 ya kukutwa, makosa mawili ya kukutwa na risasi na kosa moja la utakatishaji fedha.

Mtuhumiwa huyo amesomewa mashtaka yake na Wakili serikali Mkuu, Paul Kadushi akisaidiana na Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizire.

Aidha, katika shtaka la kukutwa na nyara za serikali, mtuhumiwa anadaiwa alitenda kosa hilo mnamo Oktoba 30, 2018 maeneo ya Oysterbay Dar es Salaam ambapo alikutwa na meno 6 ya tembo yenye thamani ya Tsh. Milioni 103.

Kosa jingine ni kukutwa na nyama ya Nyati yenye uzito wa Kilogramu 65 na thamani ya Tsh. Milioni 4.35 bila kuwa na kibali, ambalo pia alilitenda Oktoba 30, 2018 maeneo ya Oysterbay, Kinondoni Dar es Salaam.

Katika shtaka jingine, mtuhumiwa anakabiliwa na kosa la kukutwa na risasi 2404, kosa ambalo anadaiwa kulitenda Oktoba 30,2018 maeneo ya Oysterbar, Dar es Salaam.

Kosa jingine ni kukutwa na silaha aina ya Pistol, ambalo nalo alitenda Oktoba 30,2018 maeneo ya Oysterbay Dar es Salaam bila kuwa na kibali cha Msajili wa Silaha.

Kosa jingine ni utakatishaji fedha wa Dola za Kimarekani 9,018 ambalo alilitenda Oktoba 30,2018 huku akijua fedha hizo ni zao la kujihusisha na makosa tangulizi.

Baada ya kusomewa makosa hayo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, mshtakiwa amerudishwa rumande, kesi imeahirishwa hadi November 12, 2018.

Comments are closed.