The House of Favourite Newspapers

Meddie Kagere ampagawisha Kahata Simba

FRANCIS Nyambura Kahata amethibitisha kwamba mazungumzo yake na Simba yamekamilika kwa asilimia 95 na anafurahia kuungana na Medie Kagere.

 

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema tayari mchezaji huyo tegemeo wa Gormahia aliyeshindwa kuwika kwenye Afcon, ameshasaini mkataba na Simba akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa.

 

“Ni raha sana kujiunga tena na Kagere ambaye nilikuwa na wakati mzuri sana nae tulipokuwa Gormahia, ni straika mzuri sana na nadhani kucheza nae Simba itakuwa hamasa kubwa sana kwangu,”aliongeza Kahata ambaye hata
kiungo wa zamani wa Simba, Hillary Echessa amekiri kwamba Mnyama atatisha.

Kahata tayari alikuwa amemaliza mkataba wake na Gormahia ambayo ni miongoni mwa klabu kongwe za Kenya ambazo inadaiwa zimeyumba kiuchumi.

 

“Sijasaini mkataba lakini makubaliano yamefikia asilimia 95,nasubiri tu kusaini makaratasi,”alisema Kahata ambaye ni Mkenya.

Comments are closed.