MELI YA JESHI LA CHINA KUTOA MATIBABU NCHINI
MELI ya jeshi la majini kutoka China (Navy) na ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani, imeingia nchini ili kutoa matibabu ya bure kwa siku tano kuanzia kesho hadi Ijumaa Novemba 24 mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari baada ya kutembelea meli hiyo na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa ndani yake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amelipongeza jeshi hilo kwa kuiletea Tanzania huduma hiyo bora na ya bure.
Alisema hayo yote ni matokeo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili ulioanza muda mrefu na jeshi hilo ni miongoni mwa taasisi zinazoendelea kuuimarisha.
Makonda amewataka Watanzania kufika kwenye meli hiyo kuanzia kesho ili waweze kunufaika na matibabu ya bure hasa wale wanaosumbuliwa na magonjwa sugu, yenye kuwaletea matatizo kila mara na mengine yanayowasibu.
NA DENIS MTIMA/GPL