The House of Favourite Newspapers

Meneja Global Akabidhi Hundi ya Milioni 7 Kwa Wauza Magazeti

0

1.Meneja wa Global Publishers,Abdalalah Mrisho akiwakabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni saba.

3

Meneja wa Global Publishers, Abdalalah Mrisho akiwakabidhi wauza magazeti mfano wa hundi ya shilingi milioni saba.

2.Wauzaji wa magazeti wakishikilia mfano wa hundi hiyo.

Wauzaji wa magazeti wakishikilia mfano wa hundi hiyo.

 5.Laurence akizungumza jambo. 6.Mhasibu wa Global, Laurence Kabendende akizungumza na mawakala wa magazeti pamoja na wauzaji.

Mhasibu wa Global, Lawrence Kabende akizungumza na mawakala wa magazeti pamoja na wauzaji.

7.Mmoja wa mawakala akichangia hoja kwenye hafala hiyo.

Mmoja wa mawakala akichangia hoja kwenye hafla hiyo.

8.Hafla hiyo ikiendelea.

10.Hafla ikiendelea.

Hafla hiyo ikiendelea.

9.Wachangiaji wa hoja wakiendelea kutoa maoni yao.

Wachangiaji wa hoja wakiendelea kutoa maoni yao.

 11.Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallaha Mrisho akizungumza jambo katika hafala hiyo.

Meneja Mkuu wa Global Publishers,  Abdallah Mrisho akizungumza jambo katika hafla hiyo.

13.Laurence Kabende (kushoto) akiwakabidhi baadhi ya viongozi wa saccos hiyo hundi halisi ya shilingi milioni saba.

Lawrence Kabende (kushoto) akiwakabidhi baadhi ya viongozi wa Saccos hiyo hundi halisi ya shilingi milioni saba.

14.Wakiwa katika picha ya pamoja na hundi halisi ya shilingi milioni sita.

Wauza magazeti wakiwa katika picha ya pamoja na hundi halisi ya shilingi milioni saba.

15.Wakifurahia hundi hiyo.

…Wakifurahia hundi hiyo.

MENEJA wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho leo Jumatatu amekabidhi hundi ya shilingi milioni saba kwa Umoja wa Wauza Magazeti Dar, ulioanzisha (Saccos) yenye lengo la kuweka na kukopa ili kujikwamua kiuchumi baada ya uzinduzi rasmi wa Saccos hiyo uliozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda miezi kadhaa iliyopita.

Hafla hiyo imefanyika leo katika Hoteli ya The Atriums, Sinza-Afrika Sana jijini Dar es Salaam ambapo mawakala na wauzaji wote wa jijini Dar walihudhuria hafla hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Abdallah Mrisho alisema ni muhimu kwa chama kikubwa kama cha wauza magazeti kuhakikisha umoja wao wa kuweka na kukopa unakuwa imara ili uwawezeshe kujikwamua kiuchumi na kuongeza kwamba waendelee kujiunga watu wengine kupanua wigo.

Aliongeza kampuni ya Global Publishers imetoa kiasi cha shilingi milioni 7 kama kianzio cha mfuko huo ambacho alikiahidi  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Eric Shigongo.

Naye Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Abdulrahman Kapaka alishukuru Kampuni ya Global Publishers  Ltd kwa sapoti kubwa ya kuweza kuchangia chama chao hicho kwani lengo lao ni kutaka waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza kuwa watahakikisha Saccos hiyo inakua ili kuondokana na shida walizokuwa wakikabiliana nazo.

 

Leave A Reply