The House of Favourite Newspapers

ads

Messi Abakishwa PSG Apokea Ofa ya Mkataba Mpya, Barcelona Yatajwa

0
 Lionel Messi

INAELEZWA kuwa, Lionel Messi amepokea ofa ya mkataba mpya ndani ya Paris Saint-Germain, huku ikibainishwa kwamba staa huyo hajaomba mshahara sawa na ule wa Kylian Mbappe.

Messi anatarajiwa kumaliza mkataba wake ndani ya Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu.

Inaelezwa kuwa, Paris Saint-Germain inapambana kumbakiza hapo huku kukiwa na taarifa kuwa Barcelona inataka kumrejesha ingawa kuna ugumu fulani.

Paris Saint-Germain inatajwa kuwa tayari imeweka ofa ya mkataba mpya mezani.

Lakini inaelezwa kuwa, Messi hajasaini mkataba mpya kwani kwanza anataka kuelewa projekti yao kabla ya kufanya maamuzi baada ya kufanya mazungumzo ya awali Desemba mwaka jana.

Ingawa inaelezwa kuwa, kuna uwezekano mkubwa Messi akaendelea kubaki ndani ya Paris Saint-Germain.

Kocha wa Paris Saint-Germain, Christopher Galtier, alisema: “Ni mapema sana kuzungumzia mkataba mpya wa Messi.

“Najua kuwa Leo (Lionel Messi), uongozi na rais watakuwa wanalijadili hilo, lakini naweza kusema msimu ujao Leo atakuwa hapa na namuona akiwa na furaha.”

AHMED ALLY – ”YANGA ALIKULA GOLI 6, HOROYA AMEKULA PUMZI za MOTO, CHAMA NI MCHEZAJI BORA”…

Leave A Reply