Kartra

Metacha: Ilikuwa Lazima Niondoke Yanga

ALIYEKUWA mlinda Mlango wa Yanga, Metacha Mnata amefunguka kuwa ilikuwa ni lazima kuachana na kikosi hicho, kwa kuwa huo ndio ulikuwa uamuzi wenye maslahi mapana kwa pande zote mbili.

 

Metacha ambaye amehudumu kwa misimu miwili ndani ya Yanga, aliachana rasmi na timu hiyo Jumatatu iliyopita, kufuatia taarifa rasmi kutoka Yanga ikieleza kuachwa kwa makipa Metacha pamoja na Mkenya, Faroukh Shikalo.

 

Yanga imewaacha Metacha na Shikalo baada ya kukamilisha usajili wa makipa wawili, Djigui Diara raia wa Mali, na Mzawa Erick Johora aliyekuwa akiichezea Aigle Noir ya Burundi.

 

Akizungumzia ishu ya kuachwa Yanga, Mnata amesema: “Ilikuwa ni lazima kwangu kuachana na Yanga kwa kuwa tulikaa na kuangalia maslahi mapana ya pande zote mbili, na tuliachana kwa amani bila kuwa na sintofahamu yoyote kati yetu.

 

“Kuhusiana na wapi ninaelekea msimu ujao, hilo ni jambo ambalo liko chini ya Meneja wangu, Jemedari Said yeye akimaliza mazungumzo na ofa zilizo mezani mimi nitasaini na kuweka wazi.”


Toa comment