The House of Favourite Newspapers

Meya Ilala Akabidhi Vyakula kwa Wajane Vingunguti

0

MEYA WA Jiji la Ilala, Dar es Salaam Omary Kumbilamoto kwa kushirikiana na taasisi ya Alif Tanzania amekabidhi vyakula kwa familia 78 za wajane kutoka kata ya Vingunguti Jijini Dar es salaam.

 

Taasisi ya Alif Tanzania ambayo makoa makuu yake yapo nchini Uingereza kwa kushirikia na Meya wa Jiji imeweza kutoa, Mafuta ya kula mchele, unga wa sembe, unga wa ngano, sukari na tambi.

Aidha  Kumbilamoto ameipongeza Taasisi ya Alif Tanzania kwa kuamua kutoa chakula kwa Familia hizo za Wajane kwani ni watu wachache ambao wanakuwa na moyo huwo wa kutoa.

” Niwapongeze sana ndugu zangu wa taasisi ya Alif Tanzania mmeamua kuwekeza kwa Mungu huu ni msaada mkubwa sana kuwapa wajane hawa chakula hichi, Mungu awabariki sana” Alisema Kumbilamoto.

“Nitoe wito kwa taasisi nyingine kuwekeza kwa watu wenye huitaji pamoja na wajane kwani kufanya hivyo tutakuwa tumeweza kuzisaidia kaya nyingi zenye huitaji” Alisema  Kumbilamoto.

 

Mkurugenzi wa taasisi ya Alif Tanzania Shekhe Alif amepongeza  Omary Kumbilamoto kwa kuwa Meya wa Jiji na kuomba kuendelea kushirikiana zaidi hasa katika kuwasaidia watu wenye huitaji,

” Tunakupongeza kwa kuwa Meya wa Jiji sasa tunatambua majukumu yameongeza lakini pia tuomba ushirikiano zaidi ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu wenye huitaji hasa makundi kama haya ya wajane” Alisema Shekhe Alif.

Leave A Reply