The House of Favourite Newspapers

Meya wa Dar Atuma Salamu za Pasaka kwa Wananchi Wake

0

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Charles, ametuma salamu za Pasaka kwa wananchi wake na kuwataka waumini wote wa Dini ya Kikristo, kusherehekea kwa amani Sikukuu ya Pasaka na kuwataka wayatumie mapumziko hayo kulijenga jiji lao badala ya kulibomoa.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari, meya ameeleza kufurahishwa kwake na jinsi anavyoungwa mkono na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam tangu alipochaguliwa kushika wadhifa huo na kuwaahidi kwamba ataendelea kushirikiana nao kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa la kuvutia.

Meya ameeleza kwamba atahakikisha maendeleo yanapatikana na kuondokana na changamoto mbalimbali zinazolikabili jiji.

Naomba tuendelee kushirikiana na mzidi kuniombea niweze kufanya kazi ambazo mmenituma katika jiji letu. Ni wazi mnafahamu kwamba, maendeleo ya jiji letu, bila ya nyie wananchi kuonesha ushirikiano kwa viongozi wenu ambao mmetuchagua kuanzia ngazi za mitaa, kata na halmashauri hatuwezi kufika,” alisema.

Amefafanua kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa na mipango mingi mizuri ambayo imelenga kuboresha maendeleo ya wananchi wake na inaendelea kusimamia ili kuhakikisha kwamba wananchi wake wanapata huduma mbalimbali za kijamii kwa uhakika.

Amehitimisha salamu zake kwa kutoa rai kwa wakazi wote wa jiji, kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa amani na utulivu bila kuwepo kwa vurugu zozote huku salamu hizo akisema ziwe chachu ya kuendelea kutunza amani kwa kuhakikisha eneo ambalo watoto wao watashiriki kwa namna moja ama nyingine kuwe na usalama wa kutosha.

Leave A Reply