The House of Favourite Newspapers

Meya wa Ubungo ataja sababu za kutoongozana na RC Makonda, Asema Siyo Bosi Wake!

meya-wa-ubungo-jacob-1

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (kulia) akiingia kwenye ofisi za Global Publishers, kushoto ni Mhariri wa Gazeti la Ijumaa wikienda, Sifael Paul akimpokea.

meya-wa-ubungo-jacob-2

Meya Jacob akiwa mapokezi na Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kulia) na Ofisa Uhusiano wa Global Publishers, Sudi Kivea.

meya-wa-ubungo-jacob-3

Meya Jacob akizungumza wakati wa mahojiano na Global TV Online.

meya-wa-ubungo-jacob-4

Meya akifafanua jambo.

meya-wa-ubungo-jacob-7

Akiendelea kutoa ufafanuzi.

meya-wa-ubungo-jacob-8

  Meya Jacob akiwa Elvan Stambuli.

meya-wa-ubungo-jacob-16

…Katika picha ya pamoja na Mhariri Kiongozi wa Gazeti la Championi, Saleh Ally.

meya-wa-ubungo-jacob-12

…Katika picha ya pamoja na Sifael Paul.meya-wa-ubungo-jacob-10

…..Akiwa na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist

meya-wa-ubungo-jacob-11

  

meya-wa-ubungo-jacob-15

…Akiwa na Mhariri mwandamizi, Walusanga Ndaki.

meya-wa-ubungo-jacob-17

Meya akisalimia na wafanyakazi wa Global Publishers.

meya-wa-ubungo-jacob-18

DAR ES SALAAM: Meya wa Manispaa Mpya ya Ubungo, na Diwani wa Kata ya Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Boniface Jacob amesema kuwa hakuongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katika ziara yake ya Kampeni ya Dar Mpya kwa sababu wapinzani wamekuwa wakitengwa na serikali kuu.

Akifanya mahojiano maalum na Global TV Online leo Desemba 27, 2016, Meya Jacob alisema kiutendaji mkuu wa mkoa hawezi kuingilia shughuli za Halmashauri ya Manispaa, hivyo hakuona sababu ya kufuatana naye katika kampeni zake kwa sababu utekelezaji wa kero za wananchi uko mikononi mwake (meya).

“Shughuli zote zinazohusu fedha, hutolewa na halmashauri ya manispaa, hivyo alipokuwa akiwauliza wananchi kero zao, mtatuzi ni mimi na madiwani wangu, sikuona sababu ya kufuatana naye kwa sababu wanatutenga,” alisema.

“Kila kiongozi ana staili yake ya kuongoza, hivyo mimi na Makonda tunatofautiana sana staili ya kuongoza. Kwanza mimi nimechaguliwa na wananchi, haiwezekani nikaenda tena kwa wananchi kuwauliza kero zao, inatakiwa wakati nafanya kampeni ili nichaguliwe, niwe nazifahamu kero zao, hivyo nikiingia kuwaongoza ninaanza kutatua kero na siyo kuwauliza kero zao.” Alisema Meya Jacob.

“Kiutendaji na kisheria mkuu wa mkoa Siyo bosi wangu, wala hakuna kipengele cha sheria ambacho kinataja kwamba mkuu wa mkoa anaweza kuwa bosi wa meya wa manispaa, mimi siwajibiki kwake, wala yeye hawezi kuingilia kazi zangu nami pia siwezi kuingilia kazi zake.” Alieleza Meya jacob.

Akizungumzia utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli, meya huyo alisema hafikirii kama kutakuwa na maendeleo yoyote kwa sababu ya utengano unaooneshwa na serikali yake.

“Wapinzani ndio kioo cha serikali, sasa kama unakataa na kuwatenga huwezi kuleta maendeleo, ukivunja kioo chako huwezi kuona ni wapi umependeza na wapi hujapendeza. Sisi kazi yetu ni kuonesha wapi pana madhaifu ili serikali iweze kupashughulikia ipasavyo na kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Kwa njia hii inayotumika sasa na kuwazuia wapinzani kutoa mawazo, hatuwezi kupata maendeleo,” alisema.

Mbali na hayo, Meya Jacob alijivunia ukusanyaji mzuri wa fedha wa manispaa yake kwani alisema kwa mwaka wanakusanya shilingi bilioni 36 ambazo watazitumia kwa maendeleo ya wananchi.

Kuyapata mahojiano haya endelea kufuatilia channel yetu ya Global TV Online

Comments are closed.