The House of Favourite Newspapers

Mfalme Charles Mumbere wa Uganda Afunguliwa Mashtaka kwa Mauaji ya watu 62

_92715654_72629d69-f8b2-4d48-81c3-f4747451a122

UGANDA: Charles Wesley Mumbere, ambaye ni mfalme kutoka magharibi mwa Uganda amefunguliwa mashtaka ya mauaji kufuatia mapigano ya mwishoni mwa wiki ambapo utawala unasema kuwa watu 62 waliuawa.

Anatawala katika ufalme ya kitamaduni kwenye milima ya Rwenzori umbali wa kilomita 340 magharibi mwa mji mkuu Kampala. Wafuasi wake ambao ni jamii ya Bakonzo wamesambaa kutoka nchini Uganda hadi nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Msukosuko umekuwa mkubwa kwenye ufalme huo miaka ya hivi karibuni huku mizozo ya ardhi ikisababisha migawanyiko kuhusu mipango ya kuigawanya kasese, moja ya wilaya saba zilizo eneo la Rwenzori.

Sasa mfalme Mumbere na baadhi ya wafuasi wake wamelaumiwa kwa kupanga kubuni vuguvugu la kujitenga na kuunda taifa jipya kwa jina Yiira.

Hata hivyo ufalme huo umekana madai hayo.

Charles Mumbere alitawazwa kuwa mfalme wa Rwenzururu mwaka 2009, bbada ya kuishi na kufanya kazi nchini Marekani kwa miaka mingi.

Comments are closed.