The House of Favourite Newspapers

Mfalme wa Cocaine wa Milan Arudishwa Italia Baada ya Kukamatwa Brazil

0
Rocco Morabito akiwa chini ya ulinzi baada ya kurudishwa nchini Italia kutoka Brazil

MMOJA wa watu wanaosakwa sana nchini Italia, Rocco Morabito, amelabidhiwa kwa serikali ya Italia huko Roma baada ya kusafirishwa kutoka Brazil, alikokuwa amejificha.

 

Morabito    anajulikana kama “Mfalme wa Cocaine wa Milan”, alikamatwa Mei mwaka jana katika operesheni ya pamoja ya polisi wa Brazil na Italia.

 

Morabito mwenye umri wa miaka 55 atatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa ulanguzi wa dawa za kulevya Bosi huyo wa mafia alitumia miongo kadhaa kukimbia akitumia kitambulisho ghushi huko Amerika Kusini.

 

 Polisi wa Brazil walianzisha msako mkali mwaka jana katika mji wa João Pessoa, mji wa bandari kaskazini-mashariki mwa Brazili, ambako alikamatwa pamoja na mwanachama mwingine wa kundi la ‘Ndrangheta mafia, Vincenzo Pasquino.

Morabito hivi karibuni alijipatia umaarufu kama mlanguzi wa dawa za kulevya huko Milan, akianzisha njia kuu za magendo ya kokeini kutoka Amerika Kusini hadi Italia.

 

Leave A Reply