The House of Favourite Newspapers

Mgombea urais TLP ashindwa kupiga kura

0

LIMOOOOOOOOOO

Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Maximillian Lyimo.

Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Maximillian Lyimo ameshindwa kupiga kura leo katika Kituo cha Njia Panda Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro baada ya kukosekana taarifa zake kituoni hapo.

Lyimo aliyejiandikishia mkoani Dar es Salaam, jana alienda kufunga kampeni zake Jimbo la Vunjo na kulala huko, asubuhi ya leo alienda kituo cha Njia Panda jimboni humo ili akapige kura.

Baada ya kufika kituoni hapo akiwa na kitambulisho chake cha kupigia kura, alizuiwa baada ya kukosekana fomu namba 19 ambayo kisheria inamuwezesha mgombea urais kupiga kura ya kumchagua rais kwenye kituo chochote hivyo akakoswa fursa ya kupiga kura.

Leave A Reply