The House of Favourite Newspapers

Mgonjwa wa Kwanza Afariki kwa Corona Kenya

0

SERIKALI ya Kenya imethibitishia kuwa mgonjwa wa kwanza aliyekutwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini humo ambaye ni mwanamme mwenye umri wa miaka 66, raia wa nchi hiyo, amefariki dunia jana Alhamisi, Machi 26, 2020, katika Hospitali ya Aga Khan, Nairobi, alipokuwa akitibiwa.

 

Mhandisi Maurice Namiiinda mwenyeji wa Kiamlewa nchini humo, aliwasili nchini humo Machi 13, akitokea Afrika Kusini na alikuwa akisumbuliwa na Kisukari kabla ya kuambukizwa virusi vya Corona.  Alianzishiwa  matibabu lakini hali haikuimarika, hivyo kuhamishiwa kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) hadi umauti ulipomkuta.

 

 Taarifa ya kifo hicho imethibitishwa na Wizara ya Afya ya Kenya (MOH) na kuchapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Twitter wa wizara hiyo.

 

Aidha, wagonjwa wengine wapya watatu wamethibitika kukutwa na virusi hivyo na kufanya idadi ya wagonjwa wa CoronaVirus nchini Kenya kuongezeka na kufikia 31 mpaka sasa.

Leave A Reply