The House of Favourite Newspapers

MH! 50 CENT NA JASMIN BROWN KULIKONI?

0
50 Cent.

RAPA mkongwe anayewika kunako gemu ya muziki nchini Marekani, 50 Cent, ameibua maswali kwa mashabiki wake kutokana na ukaribu wake na muigizaji wa vichekesho, Jasmin Brown.
Minong’ono ya wawili hawa kuhisiwa ni wapenzi ilianza hivi karibuni baada ya kuonekana pamoja wakiponda raha katika maeneo tofauti.

Tetesi zikazidi kuchukua sura mpya tena baada ya Jasmin kuposti picha inayowaonyesha pamoja na kuimbatanisha na maneno yafuatayo:

“Najisikia vizuri kufanya kazi kila siku na bosi wangu mpya”.
Baada ya taarifa hizi kufika mezani kwa 50 Cent, amezikanusha na kusema kwamba yeye yupo ‘single’ yaani hana mpenzi yeyote kwa sasa.
NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply