The House of Favourite Newspapers

Mhandisi Mzungu Aliyezua Timbwili Mahakamani Akosa Dhamana (VIDEO)

0
Menelaos Tsampos akiwa kortini.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, le imemnyima dhamana raia wa Afrika Kusini ambaye ni mhandisi, Menelaos Tsampos, anayetuhumiwa kwa kosa la kumtishia mtu kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa kompyuta.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo wakili wa Menelaos, Deus Singa amesema;

“Kwa ujumla kesi haikuweza kuendelea, tulitegemea hakimu angeangalia kama tunakizi vigezo vya dhamana.

 

“Kama mnavyojua Menelaos anashtakiwa kwa makosa manne, kutishia kwa njia ya mtandao, kuishi nchini kinyume cha sheria na kupatikana na passport ambayo ina visa feki. Haya yote bado ni tuhuma, ili kuthibitisha unahitajika ushahidi.

“Kwa vile upande wa serikali wamesema bado wanasubili barua kutoka mamlaka ya uhamiaji, hivyo ikifika huenda kesho tukapata vigezo vya kupata dhamana,” alisema Wakili Singa.

 

Menelaos anadaiwa mahakamani hapo kuwa, Juni 22, mwaka huu maeneo ya jijini Dar es Salaam, kupitia mfumo wa kompyuta alituma ujumbe wa baruapepe (E-mail) uliokuwa na maneno ya vitisho kwa mtu anayeitwa Costa Gianna, ikiwa ni kinyume na sheria ya mtandao kifungu cha 23(1) na (2) namba 14 ya mwaka 2015.

 

Mzungu huyo aliaanzisha timbwili kortini hapo juzi baada ya kuwachimba mkwara mzito waandishi wa habari waliokuwa wakimpiga picha mahakamani hapo.

Mzungu Aliyeleta Timbwili Mahakamani Akosa Dhamana, Wakili Wake Afunguka

Leave A Reply