The House of Favourite Newspapers

Mhasibu Takukuru Akutwa na Mashtaka 44 (Video)

0
 Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Godfrey Lugai akipandishwa kizimbani.

 

Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Godfrey Lugai, jana amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, na kusomewa mashtaka 44 ya kugushi nyaraka, kutakatisha fedha haramu na kumiliki mali zenye thamani zaidi ya bilioni 3 ambazo mshitakiwa huyo ameshindwa kuzitolea maelezo ya kueleweka jambo ambalo ni kinyume na sheria za kupambana na kuzuia rushwa namba 27 cha mwaka 2006.

 

Wakili wa Upande wa Mashitaka kutoka Takukuru, Vitalis Peter alisema baadhi ya nyaraka alizogushi afisa huyo ni zile zinazoonesha kuwa viwanja vyake anavyovimiliki mikoa ya Dodoma, Tanga, Arusha, Pwani, Mwanza si mali yake na kuwataja wamiliki wengine kwenye nyaraka hizo kuwa ndiyo wanaovimiliki pamoja na mali zilizomo ikiwemo mijengo jambo ambalo si kweli.

Godfrey Lugai akipelekwa rumande.

Siku mbili zilizopita Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Generali, John Julius Mbungo, alitangaza dau nono la shilingi 10 milioni kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa Godfrey Gugai, ambaye hakuwa anajulikana alipo, lakini jana, Novemba 15, alijisalimisha mwenyewe na kuhojiwa na taasisi hiyo.

 

TAKUKURU imemfikisha mahakamani, Lugai kwa tuhuma za kumiliki mali nyingi ambazo haziendani na kipato chake jambo ambalo ni kunyume cha sheria ya Utumishi wa Umma.

 

Mali zilizotajwa kumilikiwa na Lugai ni pamoja na viwanja zaidi ya 30, magari matano, nyumba 5 na pikipiki moja ambavyo vitu hivyo viko maeneo mbalimbali hapa nchini.

Baada ya kusoma mashitaka hayo wakili wa Takukuru alimwambia hakimu aliyekuwa akisiliza kesi hiyo, Thomas Simba kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo anaomba tarehe nyingine ya kusikiliza kesi hiyo.

 

Baada ya kusema hivyo wakili anayemtetea afisa huyo na wenzake, Alex Mgongolwa aliiambia mahakama hiyo kuwa haikuwa na haja ya kusema washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu wakati maelezo ya kesi hiyo haswa shitaka la 23 mpaka 43 hayaoneshi dhana ya utakatishaji fedha haramu.

Leave A Reply