The House of Favourite Newspapers

Miaka 25 ya Chadema Karatu Bila Maendeleo, CCM Yajipanga Kuking’oa

0
Katibu tarafa Mbulumbulu Saitot Zelothe  akizungumza jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.

 

Wakati nchi ikielekea katika uchaguzi mkuu mwezi Octoba mwaka huu wanachama wa Chama cha mapinduzi wilayani Karatu wameaswa kuongeza mshikamano baina yao ili kuhakikisha chama hicho kinarudisha jimbo hilo kutoka mikononi mwa upinzani baada ya miaka 25 ambao wameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo ,ukilinganisha na maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa  Rais  Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwenyekiti UVCCM Mkoa Arusha, Omar Lumato akizungumza katika mkutano huo

 

Tangu rais Magufuli aingie madarakani serikali yake imefanya mageuzi makubwa kwenye miradi mingi ya maendeleo ambayo ilikuwa ni kero kubwa kwa wananchi ambapo wametekeleza ilani ya uchaguzi katika Nyanja ya afya, elimu, maji,umeme, mikopo kwa kina mama, vijana na watu wenye ulemavu na huduma mbalimbali za kijamii, kama walivyoahidi katika uchaguzi mwaka 2015 -2020.

Mtendaji wa kata mbulumbulu. Elikana surumbu akisoma hotuba yake katika mkutano huo.

Wakisoma taarifa za miradi hiyo inayotekelezwa na serikali ya chama cha mapinduzi maafisa watendaji wa kata za Mbulumbulu na Rothia wameeleza mafanikio ya utekelezaji wa ilani
ya chama hicho chini ya uongozi wa rais wa awamu ya tano ambayo yalikuwa ni changamoto kubwa kwa wannchi.

 

Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Mkoa wa Arusha Omary Lumato mara baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa ilani hiyo ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwa makini katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Octoba kuacha kutumika na baadhi ya wagombea kwa malengo binafsi, bali watumike kwa ajili ya chama, huku akiwataka vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati kipenga kitakapopulizwa.

Jimbo la Karatu mkoani Arusha ni moja kati ya wilaya ambazo ni ngome ya Upinzani ambapo baada ya rais Magufuli kuingia madarakani mwaka 2015 viongozi wengi wa Chadema wakiwemo madiwani walikihama chama hicho na kujiunga na CCM

Leave A Reply