The House of Favourite Newspapers

Michelle Obama Amshambulia Rais Trump

0

VITA ya maneno kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Marekani Novemba 2020, sasa imebebwa na Michelle Obama, mke wa Rais mstaafu wa taifa hilo, Barack Obama dhidi ya rais wa sasa Donald Trump, mgombea urais wa Chama cha Republican.

 

Kwenye vyombo vya habari ndani na nje ya nchi hiyo kuanzia jana jioni Jumatatu tarehe 17 Agosti 2020, Michelle ametawala kwenye vichwa vya habari kutokana na kauli yake kwamba ‘Marekani kwa Trump ilipoteza.’

 

Michelle ambaye anamuunga mkono mgombea urais wa Chama cha Republican, Joe Biden amesema, kwa miaka minne Marekani imekosa mtu sahihi wa kuiongoza.

 

Kwenye hotuba ya kampeni ya Biden iliyotolewa usiku Jumatatu kwa saa za Marekani, wanasiasa wengi walizungumza kwenye jukwaa hilo lakini hotuba ya Michelle imekuwa na nguvu kubwa na kupokelewa tofauti ndani na nje ya taifa hilo.

“Uchumi wetu unadidimia kwasababu ya virusi ambayo huyu rais alivipuuza kwa muda mrefu. Ukweli ulio wazi kwamba, maisha ya mtu mweusi ni muhimu, lakini bado ni jambo linalofanyiwa dhihaka katika ofisi ya juu.”

 

“Donald Trump sio rais sahihi kwa Wamarekani kwasababu kila tunapogeukia na kuiangalia Ikulu na uongozi wake ili tupate faraja, tunakutana na ghasia, mgawanyiko na kuchanganyikiwa kutokana na rais tusiyemuelewa kabisa.”

 

Michelle amesema, Marekani haiwezi kuwa na rais bora ambaye dhana yake ni kuonesha mtu mweupe ni bora kuliko mtu mweuzi, haiwezi kuwa na rais ambaye badala ya kuleta matumaini anasababisha ghasia na kutoelewana.

 

Amemtaja Rais Trump kama kiongozi anayetengeneza maadui kwa serikali badala ya kujenga daraja linaloweza kuwaunganisha Wamarekani wote.

 

“Viongozi wa sasa wamekuwa wakiwaita wengine kuwa maadui wa serikali, huku wakijenga dhana kwamba mtu mweupe ni bora zaidi ya mweusi.”

“Watu wamekuwa wakitupwa kizimbani huku wengine wakimwagiwa maji ya kuwasha, mabomu na hata risasi katika maandamano yanayofikisha hisia zao kwa serikali,” amesema Michelle.

 

Mwanamama huyo amewaambia Wamarekani kuwa, tayari wamemjaribu Trump na sasa, wamehakiki kuwa siye mtu sahihi anayepaswa kupewa fursa tena ya kuongoza taifa hilo.

 

“Kwa hali ilivyo, ukweli ulio wazi ni kwamba Donald Trump sio mtu yule ambaye tunaweza kumpa fursa tena. Sio mtu yute Taifa linamuhitaji. Huu ndio ukweli,” amesema.

Leave A Reply