Baba Lao! Droo ya Kwanza Shinda Gari, Washindi Waanza Kubebelea Zawadi

 

Ofisa Promosheni wa Global Publishers, Jimmy Haroub, akimvisha kitaa usoni, Shabiki wa Yanga, Anuar Mwita kabla ya kuanza kuchanganya kuponi ili achague mshindi.

DROO ya Kwanza ya Shindano la Jishindie Gari inayoendeshwa na Kampuni ya Global Group kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra imefanyika leo Jumatano, Machi 25, 2020, makao Makuu ya Group Group yaliopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam na washindi watatu kutoka mikoa mitatu tofauti wameibuka washindi kwenye droo hiyo.

Maofisa wa Kitengo cha Masoko na Usambazaji wakizimwaga kuponi eneo maalum kwa ajili ya kuchanganywa na kuchaguliwa washindi.

Droo ya kwanza ilirushwa moja kwa moja na Global TV Online na ilishuhudiwa na Mkaguzi wa Masuala ya Michezo ya Bahati Nasibu Elibariki Sengasenga. Washindi hao ni pamoja na Neema Chuma mkazi wa Kinyerezi ambaye alijishindia simu ya mkononi ambaye alisema kuwa anajivunia kuwa mwanafamilia ya michezo.

Shabiki wa Yanga, Anuar Mwita akichanganya kuponi.

 

Swaleh Mohamed (27) mkazi wa Tanga na Yesse Daniel (27), mkazi wa Moshi alikamilisha idadi ya washindi watatu wa kwanza kwenye droo hiyo ambaye ni shabiki wa Simba wote walisema kuwa wanafurahi kushinda kutokana na kushiriki mara kwa mara na kuwashauri wasomaji kuendelea kushiriki Shindano hilo.

Anuar akisoma kuponi ya mmoja wa washindi, kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally Jembe akishuhudia.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally Jembe amesema kuwa droo ya kwanza imefanyika kwa mafanikio chini ya msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Sengasenga na malengo makubwa ni kurejesha shukrani kwa wasomaji.

Anuar akisoma kuponi ya mmoja wa washindi wa Shinda Gari.

“Tumeanza na droo ndogo na zawadi bado zinaendelea kwani hatubahatishi tunafanya kwa kushirikiana na wasimamizi wa Bahati Nasibu na kuponi zilizotumika leo zitaendelea kutumika kwenye droo ya pili na Ile kubwa pia zitatumika, wasomaji waendelee kujisomea ili kupata burudani na habari,” alisema.

Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga akiipongeza Global kwa kuchezesha mchezo huo ambao una lengo la kurudisha ilichovuna kwa wasomaji wake.

Elibarik Sengasenga, Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania alisema kuwa anaewapongeza washindi wote na Kampuni ya Global Group kwa kuanzisha shindano hilo.

 

JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi au Spoti Xtra, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally akitoa neno la shukrani kwa washiriki wote wa bahati nasibu hiyo na kuwataka wengine kuendelea kushiriki kwa wingi mchezo huo.

JINSI YA KUTUMA
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

 

MASHARTI YA KUSHIRIKI
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda.
Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

LUNYAMADZO MLYUKA | PICHA: RICHARD BUKOS/GPL     

Toa comment