Lakini ahadi hii imeibua shutuma kali na kejeli kutoka kwa Wakenya mtandaoni. Takriban wanasiasa 12 tayari wameanza kampeni za kumrithi Rais aliye madarakani Uhuru Kenyatta, ambaye yuko katika miezi ya mwisho ya miaka 10 madarakani.
Miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ni kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga na Naibu Rais wa sasa William Ruto, ambao wanaonekana kuwa wagombea wakuu katika uchaguzi wa Agosti 2022.
Uchumi, ukosefu wa ajira kwa vijana na kupambana na ufisadi vimeibuka kuwa masuala muhimu katika ajenda za wanaowania urais, lakini chaguzi zilizopita zimeonesha kuwa Wakenya wengi hupiga kura kwa kuzingatia ukabila badala ya masuala ya sera.