The House of Favourite Newspapers

Minziro huyo arejea daraja la kwanza

0

minziro-e1415273563704Kocha Fred Felix Minziro.

Martha Mboma, Dar es Salaam

LICHA ya Klabu ya Africans Sports kuonyesha dalili ya kutaka huduma ya kocha Fred Felix Minziro na kuingia mitini ghafla, kocha huyo amefunguka kuwa huenda akarejea Ligi Daraja la Kwanza baada ya klabu za Panone FC na Geita Gold Sport kuonyesha nia ya kutaka kufanya naye kazi.

Kocha huyo ambaye alikuwa akiifundisha timu ya JKT Ruvu, aliachia ngazi baada ya mambo kuonekana magumu na kuamua kupumzika kwa muda huku msimu wa nyuma yake, akiinoa Yanga pamoja na Mholanzi, Ernie Brandts.

“Nipo tayari kurudi kufundisha hata daraja la kwanza kwa sababu kuna baadhi ya ofa nimezipata kutoka katika klabu za Panone FC ya Moshi na Geita Gold ya Geita, zinahitaji huduma yangu na mimi ndiyo kazi yangu, cha msingi ni makubaliano tu.

“Kwa upande wa African Sports ni kweli walikuwa wananihitaji, kuna baadhi ya viongozi walishawahi kunifuata awali lakini hawakuwahi kurudi tena na sifahamu kitu gani kinaendelea, hivyo pale ambapo tutakubaliana ndipo nitakwenda kufanya kazi,” alisema Minziro.

 

Leave A Reply