MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA YA UREMBO WA DUNIA 2017

Mrembo wa Tanzania aliyeteuliwa kushiriki Urembo wa Dunia, Julitha Kabete, akizungumza na wanahabari..

MISS Tanzania mteule wa mwaka 2017, Julitha Kabete,  leo amekabidhiwa bendera ya Tanzania kwa ajili ya kushiriki mashindano ya urembo ya Dunia 2017 yanayotarajiwa kufanyika Novemba 18 mwaka huu nchini China.

 

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye alikuwa ni Ofisa Utamaduni Mkuu, Habibu Msammy (kushoto) akimkabidhi Julitha bendera ya Tanzania.

Mrembo huyo alikabidhiwa bendera hiyo na  aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Ofisa Utamaduni Mkuu, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Habibu Msammy,  jijini Dar es Salaam ambapo aliwaomba Watanzania wamtakie kila mafanikio Julitha katika mashindano hayo yajayo.

 

Baadhi ya viongozi wanaoandaa safari ya mshiriki huyo wakiwa katika picha ya pamoja.

Akitoa shukurani zake, mnyange huyo pia alisema atafanya juu chini kuhakikisha anapata ushindi kutokana na kuwa na maarifa mengi kuhusiana na mashindano ya urembo aliyoyapata hapa nchini  ikiwa pamoja na Nigeria mwaka 2016.

“Nikiwa nimeanza kushiriki mashindanoya urembo kuanzia kituo cha Dar City Centre, Miss Ilala na hatimaye fainali za Miss Tanzania 2016,   nimeweza kujifunza mambo mengi katika tasnia hii ya urembo, hivyo mtegemee nitaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwani nimewahi kushiriki mashindano ya urembo ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria mwaka 2016,” alisema Julitha.

NA DENIS MTIMA/GPL


Loading...

Toa comment