The House of Favourite Newspapers

Miundombinu ya Barabara Polisi Mabatini, Dar… Sikio la Kufa!

0

1.Gari likipita eneo hilo kwa tabu.Gari likipita eneo hilo kwa tabu.

2.Bajaj nayo ikipita kwa tabu. Bajaj nayo ikipita kwa tabu.

Mjumbe wa Mtaa wa Polisi Mabatini, jijini Dar es Salaam,  Steven Jovin amesema kuwa barabara ya Kijitonyama (Polisi Mabatini) anaifananisha na sikio lisilosikia dawa kwa kuwa amelalamika sehemu mbalimbali hadi amecho.

4.Taswira ya eneo hilo kama inavyoonekana.Dereva Bodaboda naye akiikwepa sehemu hiyo mbovu.

Akizungumza na mwandishi wetu, Jovin alisema kuwa imekuwa kero kubwa ya muda mrefu kwa barabara hiyo ambayo ina dimbwi kubwa la maji pasipo kurekebishwa hali inayosababisha magari kupita kwenye makazi ya watu na kuharibu miundombinu ya maji na mazingira.

5.Baadhi ya gari zikikwepa kupita eneo hilo bovu.Baadhi ya gari zikikwepa kupita eneo hilo bovu.

“Meya wa Manispaa ya Kinondoni alishafika  eneo hili kuangalia lakini bado sijaona wakandalasi wakifika kutengenza barabara hii hasa eneo hili walau kwa kuweka vifusi,” alisema.

6.Gari na Bajaj zikiendelea kupita kwa tabu.Gari na Bajaj zikiendelea kupita kwa tabu.

Akaongeza: “Kila siku vyombo vya habari vinakuja hapa kuchukua tukio hili sijui wahusika hawaoni jamani, naiomba watu wanaohusika waliangalie hili,” alisema Jovin.

3.Dereva Bodaboda naye akiikwepa sehemu hiyo mbovu.Taswira ya eneo hilo kama inavyoonekana.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply