The House of Favourite Newspapers

MJANE ATUPIWA VIRAGO, AMWANGUKIA MAGUFULI NA MAKONDA

Eneo la nyumba inayodaiwa alikuwa akiishi Editha Wambura likiwa limewekewa tepe za kutoruhusiwa tena kuingia ndani yake.
Wambura akiwa na mwanaye.

 

MJANE aliyejitambilisha kwa jina la Editha Wambura mkazi wa Mikocheni-Viwandani, Dar es Salaam, ambaye amedai alikuwa mmiliki wa Klabu ya Msasani kabla ya kudhulumiwa na ndugu,  amemwangukia Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wamsaidie katika mgogoro na familia yake uliosababisha kampuni moja ya udalali jijini hapa, kumwondoa ndani ya nyumba aliyodai niyakwake.

 

Wambura, mama wa watoto watatu ambaye amesema alikuwa akiishi katika nyumba hiyo kabla ya kifo cha mume wake na kabla hawajapata watoto hao.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, mwanamke huyo ameeleza kuwa migogoro ilianza mara baada ya kufariki mmewe na  aliporudi kutoka kumzika mume wake ambapo ndugu wa mume huyo walianza kugombania mali zake wakitaka kugawana naye, jambo ambalo hakukubaliana nalo.  Na alivyopeleka malalamiko yake kwenye vyombo vya haki, hadi sasa suala hilo halijapatiwa ufumbuzi wakati ni muda mrefu umepita.

 

Akizungumza zaidi, amesema ndugu wa marehemu mumewe wamekuwa wakileta wanawake ‘feki’ wenye watoto kwa lengo la kugawana nao mali za mumewe kwa madai ni watoto wa marehemu.

 

Mlalamikaji huyo aliongeza kwamba mali alizoacha mumewe, ikiwa ni pamoja na fedha, Klabu ya Msasani na vinginevyo, vyote vimedhulumiwa na ndugu.

 

Comments are closed.