The House of Favourite Newspapers

Mkali Wenu: Alikiba Aliniomba Kumwandikia ‘Mediocre’

0

MCHEKESHAJI maarufu nchini, Mkali Wenu,  ametoa kali ya mwaka baada ya kufunguka kwamba alimwandikia wimbo wa Mediocre  msanii Alikiba ambapo amesema awali wimbo huo alitaka ampatie Nay wa Mitego ila aliishindwa.

 

“Kitu chochote kinaweza kutokea, kama menejmenti yangu ikisema nifanye kazi na Alikiba nitafanya naye, kwa sababu Alikiba ni mshkaji wangu na namwandikia nyimbo, hata hii nyimbo aliyotoa ya Mediocre nilikuwa nayo muda mrefu aliniomba nikamwandikia, ukiangalia ina utofauti na nyimbo zake zingine,” amesema Mkali Wenu.

 

“Kumwandikia mtu haimaanishi kama hauna sauti ila Alikiba yeye ana sauti nzuri, mimi nina sauti ila sio nzuri kwenye kuimba, nyimbo ya Mediocre imekaa vizuri kwake nilishawahi kumpa Nay wa Mitego akasema haiwezi kuiimba…”

 

Aidha, amesema ‘role model’ wake alikuwa ni marehemu Sharo Milionea ambaye alianzia kwenye uchekeshaji kisha kuimba, hivyo watu wasishangae kumwona na yeye akianza kuimba.

Leave A Reply